Beki mpya aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni akitokea JKT Ruvu,
Mohammed Faki, amekwaa kisiki katika kikosi hicho cha Wanamsimbazi, baada ya
jezi ya namba aliyokuwa akiihitaji kuwa na mtu.
Faki amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili ambapo
alikuwa akiihitaji jezi yenye namba 26 ambayo alikuwa akiivaa tangu alipokuwa
Ashanti United na JKT Ruvu, lakini katika kikosi cha Simba, inavaliwa na
nahodha, Hassan Isihaka.
Faki amesema kwa kuwa bado hajakabidhiwa jezi tangu asajiliwe
Jumatano ya wiki iliyopita, lakini kama angekuta jezi namba 26 haina mtu, basi
ingekuwa mali yake.
Aliongeza kuwa, kutokana na jezi hiyo kuvaliwa na Isihaka, hana
budi kuchukua nyingine huku akishindwa kutaja namba gani kutokana na ile anayoipenda
kuwahiwa mapema huku akisema yupo tayari kuvaa yoyote.
“Ningekuwa na uwezo basi ningeuomba uongozi unipe jezi namba 26
kwani nimetokea kuipenda tu ambapo tangu nilipokuwa Ashanti na JKT Ruvu
nilikuwa naivaa lakini nimekuja huku nimekuta tayari ina mtu.
“Siwezi kumwambia Isihaka aniachie kwani najua na yeye anaipenda,
hivyo nipo tayari kuchukua yoyote ile na nitaikubali kwani sina jinsi tena,
baada ya ile niliyokuwa naipenda kuwa na mtu,” alisema Faki.
0 COMMENTS:
Post a Comment