Kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke, ametamka wazi kuwa, anaishukuru klabu yake hiyo mpya kwani
imechangia kwa kiasi kikubwa yeye kuongezwa katika kikosi cha Taifa Stars
kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Kaseke ambaye ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea
Mbeya City, hivi karibuni aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Stars
kinachonolewa na Mholanzi, Mart Nooij, sambamba na wachezaji Said Mohammed, Vincent
Andrew ‘Dante’ wa Mtibwa Sugar na Benedict Tinoko wa Yanga.
Kaseke amesema kuwa bila ya Yanga kumsajili, kusingekuwa na
uwezekano wa yeye kuitwa Stars kwa sababu mara nyingi kikosi hicho kimekuwa
kikiundwa na wachezaji wengi wanaozichezea klabu za Dar, tofauti na mikoani
licha ya wachezaji wengi wa timu za mikoani kuwa na uwezo wa kucheza katika
kikosi hicho.
“Kiukweli kabisa napenda kutoa shukrani kwa viongozi wa timu ya
Yanga kwa kuweza kuchangia kwa namna moja au nyingine mimi kuitwa katika kikosi
cha Stars, kwani bila ya kuwepo hapa (Dar), ingekuwa ngumu kwangu kuwemo katika
kikosi hicho, licha ya kuona nina uwezo wa kukitumikia kikosi hicho kwa kipindi
kirefu sasa.
“Nahisi kama nisingekuwa Yanga sasa, ningekuwepo Stars kutokana na
wachezaji wengi wanaoitwa ndani ya kikosi hiki kutokea katika timu za hapa Dar,
tofauti na mikoani,” alisema Kaseke.
0 COMMENTS:
Post a Comment