Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameuambia
uongozi wa Yanga kwamba anataka wachezaji wenye kasi katika kikosi chake.
Kutokana na mfumo anaotaka kuucheza, Pluijm anaamini
Yanga inataka wachezaji wenye kasi kubwa.
“Kocha anataka wachezaji wenye kasi zaidi, hivyo
tumemuachia mwenyewe ajipange katika hilo.
“Ndiyo maana mlisikia anaweza kuja na mawinga wawili,
siku hizi mnasema viungo wa pembeni. Anaangalia wenye kasi.
“Kama atakuja na mmoja, bado Yanga ina wachezaji
wengine wenye kasi,” kilieleza chanzo.
Yanga imetenga nafasi ya wachezaji wawili wa kimataifa
na imeelezwa nafasi za Coutinho na Kpah Sherman ambao imeelezwa, ndiyo safari
imewakuta.
0 COMMENTS:
Post a Comment