Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Benki
ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Jana
kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa
Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa
mazoezi.
Taifa
Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na
mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi
ya timu ya taifa ya Misri.
Daktari
wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa
maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika
ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji
kuwa fit kwa ajili ya mchezo.
Hali
ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa
na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini
hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kwa ajili ya mchezo”
Alisema Haonga”.
Wachezaji
wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya,
kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.
Wenyeji
Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata
mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment