July 10, 2015

MWINYI
Mara baada ya kujiunga na Yanga, beki mpya wa pembeni wa timu hiyo, Haji Mwinyi Mngwali, ameomba jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na Mganda, Hamis Kiiza aliyetua Simba.


Kiiza aliiacha jezi hiyo baada ya mkataba wake kusitishwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, msimu uliopita.

Haji ambaye ni beki wa kushoto ambaye atakuwa akiwania namba na Oscar Joshua, ametua kuichezea klabuni hapo akitokea KMKM inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.

Haji aliivaa jezi hiyo juzi kwa mara ya kwanza katika mechi ya kirafiki ya Yanga dhidi ya KMKM kwenye Uwanja wa Taifa ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Donald Ngoma.

 Haji amesema: “Nimeona hii jezi ndiyo inayonifaa, hakuna mtu aliyenishawishi kuivaa, niliiomba baada ya kuambiwa kuwa hakuna mchezaji anayeivaa, hivyo nikaona niichukue niivae.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic