Klabu ya Simba sassa mambo yao safi
baada ya fedha Sh milioni 220 kuingia katika akaunti yao.
Fedha hizo ni malipo ya mauzo ya
mshambuliaji Emmanuel Okwi Arnold kwenda katika klabu ya Sonderjyske ya nchini nchini Denmark.
Sonderjyske
ilikubali kulipa dola 110,000 ili kumnasa Okwi. Ikaahidi kulipa fedha hizo Juni
17 na imechelewa kidogo tu lakini imeweza kutimiza ilichoahidi.
Habari
za uhakika kutoka Simba, zimeeleza kuwa Sonderjyske imeilipa Simba kupitia
akaunti yake ya CRDB jijini Dar es Salaam.
“Kweli
Simba wamelipwa fedha zao, lakini ni suala ambalo viongozi hawawezi
kulizungumzia kwa sasa,” kilieleza chanzo.
Tayari
Okwi yuko nchini Denmark katika kikosi chake cha Sonderjyske akiendelea
kuitumikia timu yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment