Mshambuliaji Hamisi Kiiza amesaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ya Dar es Salaam.
Kiiza amesaini mkataba huo baada ya
kufuzu zoezi la vipimo jijini Dar es Salaam.
Kiiza ambaye ni mshambuliaji wa zamani
wa Yanga aliwasili jana akitokea nchini Uganda kwa ajili ya vipimo na kumalizia
mazungumzo na uongozi wa Simba.
Akiwa nchini, Kiiza alisema amekuja
kufanya kazi na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment