CHUJI |
Katika kuhakikisha wachezaji wake wanaimarika na kuwa na nguvu muda wote, Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amewapiga marufuku wachezaji wake akiwemo kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ kula visivyowapa nguvu mwilini vikiwemo ‘chips kuku’.
Badala yake, Julio amesema anataka kuona wachezaji wake wanaweka mkazi wa kula vyakula vya kuutia nguvu mwili vikiwemo makande na ugali wa dona.
JULIO |
Julio aliyewahi kucheza na kufundisha Simba, alisema anataka wachezaji wake wawe wapambanaji mashujaa uwanjani hivyo lazima awasimamie wale vyakula vya kujenga mwili.
“Tuna mipango mwingi ikiwemo kuweka kambi Afrika Kusini, lakini nimewaambia hakuna mtu anayeruhusiwa kula chips kuku wala chips mayai kwani havina manufaa katika miili yao,” alisema Julio.
“Unajua nimegundua wachezaji wa siku hizi wanashindwa kufanikiwa uwanjani kutokana na uvivu na aina ya vyakula wanavyokula hivyo hapa Mwadui ni marufuku chips kuku hapa ni mwendo wa ugali wa dona, makande na vyakula vya kumjenga mchezaji.”
Julio alisema kikosi chake kimesheheni wachezaji wote isipokuwa Rashid Mandawa ambaye yupo Taifa Stars na Emmanuel Semwenda mwenye matatizo ya kifamilia.
0 COMMENTS:
Post a Comment