Kocha
Mkuu wa Simba, Dylan Kerr ameuambia uongozi wa Simba ufanye kila linalowezekana
kusajili kipa mwingine.
Kerr
raia wa Uingereza amenusa mbele na kuona kipa aliyeiva katika kikosi chake ni
Ivo Mapunda pekee.
Hivyo
lazima awe na kipa mwingine iwapo itatokea dharura.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa ni kweli,
Kerr anataka kipa.
“Kweli
na tumeanza kulifanyia kazi suala hilo. Tunaendelea kusaka kipa sehemu
mbalimbali ili kutimiza hilo ombi la kocha.
“Wakati
wa michuano ya Kagame pia tutaendelea kutafuta kipa. Ni suala la kiufundi,
hivyo linahitaji utulivu, kuangalia na kushariana,” alisema Hans Poppe.
Kipa
mwingine wa Simba ni Peter Manyika ambaye alipata nafasi ya kukitumikia kikosi
hicho msimu uliopita.
Pamoja
na kujitahidi, Manyika alifanya makosa kadhaa makubwa yaliyoisababishia Simba
matatizo, lakini Simba walionyesha uvumilivu wakiamini ndiyo anajifunza.
0 COMMENTS:
Post a Comment