Mashabiki wa Yanga sasa hawatapata nafasi ya kuiona timu yao mazoezini kama walivyozoea.
Hiyo ni baada ya uongozi wa Yanga kutangaza hautaruhusu mashabiki kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo kwa siku tano.
Yanga imeingia kambini Kurasini jijini Dar es Salaam, hivyo Kocha Hans van der Pluijm ameomba apewe nafasi nzuri ya kuiandaa timu yao kabla ya michuano ya Kagame Jumamosi.
"Kweli tumeangalia kambi nzuri lakini mashabiki sasa watupe nafasi kidogo kwa ajili ya kumalizia maandalizi hayo ya mwisho," alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro.
Kawaida mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwenye mazoezi ya Yanga, wakati mwingine wakiwatuza wachezaji, jambo ambalo ni aghalabu kutokea katika sehemu ambazo soka limepiga hatua au kuendelea kwa kiwango cha juu.
0 COMMENTS:
Post a Comment