Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema hataelekeza nguvu zake
sasa katika ushindani wa kikosi chake dhidi ya Azam FC na Yanga.
Kerr raia wa Uingereza amesema hatafanya hivyo ili kuepuka
kupoteza umakini wa kukiandaa kikosi chake.
Ameshapewa taarifa za upinzani dhidi ya timu hizo, lakini anaamini
ligi ni ushindani wa timu zote.
“Nilishaambiwa na hata mimi
mwenyewe nimefuatilia kwamba hapa Yanga na Azam ndiyo wapinzani wakubwa wa
Simba na hata mechi zao huwa ngumu sana lakini sihitaji kuliangalia hilo sana
zaidi ya kutazama hizi nyingine 13 zilizobaki ambazo naamini ndizo zenye faida
zaidi kama tutafanikiwa kuwa na matokeo mazuri,” alisema Kerr.
Tayari Kerr ameanza maandalizi ya kukinoa kikosi chake mara baada
ya kuingia kandarasi ya kuinoa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment