Hatimaye Yanga na
Kimondo zimemaliza kuhusiana na mchezaji Geofrey Mwashiuya.
Katibu Mkuu wa Yanga,
Dk Jonas Tiboroha amesafiri hadi mjini Mbozi na mwisho wamefikia mwafaka.
“Kweli tulikaa kama
uongozi wa Yanga, tukaona ni jambo zuri kumalizana vizuri na Kimondo.
“Tumemalizana baada ya
kukutana nao, wakatupa wanachodai tukaangalia na mwisho tumefikia mwafaka.
“Sasa Mwashiuya ni
mchezaji wa Yanga na Kimondo wamelipitisha hilo,” alisema.
Awali, Kimondo ilikuwa
ikipinga Yanga kumsajili Mwashiuya huku wakiwataka TFF kuwa makini na
kutompitisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment