Kocha Dusan Momcilovic raia wa Serbia mtaalamu wa masuaa ya
viungo amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba.
Kazi kubwa ya kocha huyo ni kuwaweka fiti wachezaji wa kikosi cha Simba ambao watakuwa chini ya Kocha Mwingereza, Dylan Kerr na msaidizi wake, Mtanzania Selemani Matola.
Tayari kocha huyo mpya ameanza kazi jana kuinoa Simba kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment