Yanga imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Kagame
ikitokea Kundi A ikiwa ni baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM.
Katika mechi hiyo yenye kasi kubwa, Yanga ilipata ushindi huo
kupitia kwa bao la Malimi Busungu.
Kabla ya beki wa KMKM kujichanganya na Amissi Tambwe kuupiga mpira uliompita kipa
Nassor Abdullah na kuandika bao la pili.
Mpira ulikuwa wa kasi na ushindani mkubwa huku KMKM wakitoa
upinzani mkali ingawa katika dakika 30 za mwisho, walionekana kulishinda ‘rigwaride
la Yanga’.
Yanga sasa imefikisha pointi sita baada ya mechi tatu, ikiwa
imepoteza moja dhidi ya Gor Mahia.
Ita,alizia meechi ya mwisho dhidi ya Al Khartoum yenye pointi
saba, Jumapili. Iwapo itashinda itakuwa imefikisha pointi 9 na kuwa katika
nafasi ya pili au ya kwanza ingawa itasubiri pia matokeo ya Gor Mahia na
Telecom.
Katika mechi ya kwanza, Gor Mahia ilitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Al Kharthoum.
0 COMMENTS:
Post a Comment