August 26, 2015

BANDA AKITIBIWA NA DAKTARI MARA TU BAADA YA KUUMIA HUKU MSHAURI WA UFUNDI WA STARS, ABDALLAH KIBADENI AKISHUHUDIA. PIA MUDATHIR YAHYA NA HIMID MAO.
Na Saleh Ally, Kartepe
KIUNGO wa Simba, Abdi Banda anayekipiga katika kikosi cha Taifa Stars ameumia akiwa mazoezini mjini hapa nchini Uturuki.


Banda ameumia wakati wa mazoezi ya kukimbia kwa kasi yaliyokuwa yakiongozwa na Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwansa na msaidizi wake, Hemed Morocco.

Banda aliumia wakati akichuano vikali na John Bocco na Nadir haroub ‘Cannavaro’.

Hata hivyo alipewatiwa na matibabu baada ya kuondolewa mazoezini na kupumzishwa ingawa daktari wa Stars alisema anaendelea vizuri.
Stars ilifanya mazoezi mara mbili jana, ikianza asubuhi na jioni na Banda alipumzishwa.

Taarifa za kidaktari zimeeleza, huenda Banda akaanza mazoezi kesho kwa kuwa hali yake itakuwa imekaa vizuri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic