BOCCO AKIONGOZA MBELE YA BANDA NA CANNAVARO HUKU KOCHA MKUU, CHARLES BONIFACE MKWASA AKISHUHUDIA. |
Na
Saleh Ally, Kartepe
KIKOSI
cha Taifa Stars kimeendelea leo na mazoezi kwenye mji mdogo wa Kartepe huku
Kocha Boniface Mkwasa akianza na mazoezi ya kukimbia kasi.
Wachezaji
wa Stars walifanya mazoezi ya kukimbia kwa kasi na Simon Msuva, John Bocco na
Rashind Mandawa wakiibuka kidede huku wakijisifia kwamba wana kasi kama ile ya
mwanariadha maarufu wa Jamaica, Hussein Bolt.
Akisaidiana
na msaidizi wake, Hemed Morocco, Mkwasa alikuwa akiwapa nafasi ya kukimbia kwa
kasi kubwa ndani ya Mita 100.
Mara
kadhaa, Msuva aliyekuwa akijisifia kuisaka kasi ya Bolt ndiye alikuwa akiongoza
katika kundi lake.
Bocco
na Mandawa, kila mmoja aliongoza kundi lake na ndiyo waliofanikiwa kumaliza kwa
sekundu 10 hadi 11.
Pamoja
na mazoezi hayo ya kasi, pia walipata nafasi ya kuuchezea mpira, halafu Mkwasa
akawapunguza na kugawa timu zenye watu watano watano.
Mazoezi
hayo ya kama saa mbili na nusu yalimalizika saa sita kasorobo na wachezaji
walipata muda wa kupumzika kabla ya kula chakula cha saa saba na nusu na saa 10
jioni wakarejea mazoezini.
0 COMMENTS:
Post a Comment