Mara tu baadaa ya Angel Di Maria
kufuzu vipimo vya afya, neno la kwanza alilolisema ni kwamba anataka kuisaidia
PSG katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Di Maria amesema amekuwa na furaha
kubwa kwamba anajiunga na timu hiyo ya Paris Saint-Germain lakini anachotaka ni
kuona anakwenda mbali nayo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akisashaini, atakuwa mchezaji wa
pili ghali zaidi nchini Ufaransa baada ya Edinson Cavani.
Cavani alisajiliwa kwa kitita cha
euro milioni 64 wakati Di Maria itakuwa euro milioni 63.
Di Maria ameondoka Manchester
United na kuzua gumzo kubwa kwa kuwa ilionekana kama hakutakiwa kuondoka wakati
huu kwa kuwa timu hiyo ndiyo inajiweka vizuri ili kurejea katika hadhi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment