Real
Madrid imekubali kumuachia mshambuliaji wake Mfaranda, Karim Benzema, ajiunge
na Arsenal.
Lakini
imeweka wazi masharti kwamba kama kweli Arsenal iko tayari, basi ivunje rekodi
yake ya usajili kwa kutoa pauni milioni 45.
Arsenal
ndiyo iliweka rekodi ya manunuzi kwa Real Madrid baada ya kumchukua Mesut Ozil
kwa kitita cha pauni milioni 42.5, hiyo ilikuwa mwaka 2013.
Sasa
Madrid imesema hata Benzema, anaweza kuhamia London, England. Lakinia hayo
ndiyo masharti.
Hivyo
wakali hao wa Hispania, tayari wamerushia mpira upande wa Arsenal waliokuwa
wakionekana kumtaka Benzema kwa muda sasa.
Kazi
kwao kuucheza mpira huo kama kweli wanataka kumsajili Benzema ambaye hakika
bado ni kifaa na Madrid wenyewe bado wanamtegemea.
0 COMMENTS:
Post a Comment