Na
Saleh Ally, Kartepe
KIKOSI
cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kimesafiri kwa zaidi ya saa 10 hadi
katika mji mdogo kabisa wa Kartepe hapa nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka
kambi.
Kambi
hiyo ni kwa ajili ya kujiwinda ili kuwa fiti kabla ya mechi ya kuwania kucheza
Kombe la Mataifa aAfrika dhidi ya Nigeria, mechi itakayopigwa Septemba 5 jijini
Dar es Salaam.
Kabla
haitakuwa mechi ndogo na Stars ambayo kwa mara ya kwanza, mara nyingine timu
hiyo inanilewa na makocha wote wazalendo.
Safari:
Safari
ya Stars kuja hapa Uturuki ilianzia Dar es Salaam na ndege iliondoka saa 9:45
usiku na kuwasili Istanbul Uturuki saa 4:45 asubuhi ikiwa ni saa saba bila ya
kupumzika angani.
Safari
hiyo ndeefu iliwafanya wachezaji wa Stars kuonekana wakiwa wamechoka sana
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ataturk na baada ya hapo safari ya
kwenda kambini iliyochukua saa tatu na shee ilianza kwa basi.
Awali
ilionekana ni kama safari fupi tu, lakini haikuwa hivyo baada ya wachezaji
kujikuta wakisafiri kwa saa tatu kutoka Istanbul hadi katika mji wa Izmil ambao
ni wa tatu kwa ukubwa hapa Uturuki baada ya Istanbul na Ankara.
Kambi:
Bado
Stars hawahaweka kambi mjini, badala yake wamepanda katika milima iliyo nje ya
mji huo katika eneo linalojulikana kama Kartepe ambako kambi hiyo iko katika
Hoteli kubwa ya The Green Park.
Kwa
Dar es Salaam, The Green Park Hotel ni mfano wa Serena Hoteli, lakini hii ya
hapa Uturuki ni kubwa mara tatu ya Serena.
Ina
uwezo wa kupokea timu 11 hadi 14 kwa wakati mmoja. Ni hoteli ya kisasa ambayo
inajumuisha nyumba maalum za kupanga maarufu kama apartment.
Hoteli
hiyo inamiliki viwanja vitano vya kisasa vya mazoezi ambavyo timu mbalimbali
zinazifokia hapa zinavitumia kwa ajili ya kujiweka sawa.
Wakati
Stars inawasili katika kambi hiyo, timu ya taifa ya Bahrain ndiyo ilikuwa
inaondoka. Lakini timu ya taifa ya Jordan na Libya zilikuwa ni kati ya timu
zilizoweka kambi pia kulikuwa na klabu ya Al Ana’aa ya Libya ambayo pia ilikuwa
hapa kwa ajili ya kujiandaa.
Kila
wakati wa mazoezi uliopangwa na mwalimu, mabasi yamekuwa yakifika kuwachukua
wachezaji na makocha pia kuwarudisha.
Kinachovutia
zaidi, viwanja hivyo vimekuwa vikitumiwa kwa muda. Mfano kama umepangiwa kuanza
saa 5 asubuhi, basi hadi saa 6:30 utatakiwa kung’oa virago na kuwapisha
wengine.
Hali
ya Hewa:
Hali
ya hewa ya hapa ni kiboko, baridi ni kali kwa kuwa ni kuanzia nyuzi joto 12
hadi 14. Siku moja kabla ya Stars kuwasili, mvua zilinyesha mfululizo kwa saa
72.
Lakini
tokea timu imewasili hali ya hewa si ya mvua tena, lakini baridi na hasa
unapowadia usiku, inakuwa kali zaidi.
Kocha
Charles Boniface Mkwasa na msaidizi wake, Hemed Morocco pamoja na mshauri wa
masuala ya ufundi, Abdallah ‘King’ Kibadeni wanaonekana kuifurahia hali hiyo
huku kila mmoja akisema wana imani mambi yatakuwa mazuri zaidi.
Benchi
la ufundi la Stars linaamini mazoezi kwenye baridi ni bora kuliko kwenye joto
ingaw atimu italazimika kurejea Septemba Mosi ili kuzoea tena hali ya hewa ya
Dar es Salaam.
Jana,
Stars ilijifua mara mbili, lakini leo itajifua mara moja tu asubuhi, jioni
wachezaji watapumzika kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Libya ambayo
itachezwa saa tano asubuhi.
Mkwasa
amesema anapambana kuhakikisha wanaitumia mechi hiyo kama faida kwa Libya wana
kikosi bora pia na watatoa msaada yeye na wenzake kujua wapi pa kufanyia kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment