August 15, 2015

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limekiruhusu Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Soka Temeke (Tefa) kama ulivyopangwa na kamati ya uchaguzi ya  chama hicho.

Baada ya ruhusa hiyo Uongozi wa DRFA umemuandikia barua Katibu Mkuu wa TEFA, Kassim Mustapha ili aijulishe kamati ya uchaguzi ya chama hicho kuendelea na mchakato huo kama kawaida.

Awali, TFF iliiandikia barua DRFA kushauri kusimamishwa kwa uchaguzi huo,kutokana na kile kinachoonekana kuwepo na malalamiko kuhusu mchakato wake lakini maada ya mashauriano kati ya pande hizo mbili,sasa ni ruksa kwa uchaguzi huo kufanyika kesho jumapili Agosti 16,2015 kama ulivyopangwa.


Aidha, DRFA imewaomba wapiga kura wote kujitokeza kwenye uchaguzi,huku ikisisitiza amani na utulivu itawale katika zoezi hilo muhimu la kuwapata viongozi watakaokiongoza chama cha soka Temeke,ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA MSEMAJI WA DRFA, OMARY KATANGA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic