August 15, 2015


Kiungo Justice Majabvi, amesaini mkataba wa kuichezea Simba na amepiga mkwara mzito kwa viungo wenzake akiwemo Jonas Mkude kuwa wajipange la sivyo watakaa benchi.

Awali, baadhi ya viongozi wa Simba hawakutaka kabisa Majabvi asajiliwe kwa maelezo kuwa kiwango chake ni cha kawaida wakati wapo wazawa kama Mkude, Said Ndemla, Awadh Juma na Abdi Banda wanaoweza kucheza nafasi yake.

Lakini Kocha Dylan Kerr akawaambia viongozi hao: “Mimi ndiye bosi na lazima mumsajili Majabvi.” Kweli Majabvi raia wa Zimbabwe akasaini mkataba wa miaka miwili na sasa ni mali ya Simba.

Muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo, Majabvi akasisitiza: “Najipanga kikamilifu kucheza kikosi cha kwanza, nimekuta watu wanacheza hapa nami nitapambana ili nicheze, naamini hakuna linaloshindikana.


“Kwa upande wangu ninajipanga kikamilifu kuhakikisha napigana na kuonyesha uwezo wangu wa hali ya juu ambao utamshawishi kocha anipange katika kikosi cha kwanza na kuwapokonya namba hawa niliowakuta,” alisema Majabvi ambaye amewahi kuichezea timu ya Vicem Hai Phong ya Vietnam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic