August 13, 2015


Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameendelea kusisitiza kwamba ikifikia siku akamnasa mtu anayejihusisha na utoaji na upokeaji rushwa, atakuwa mfano kwa wengine wengi,.


Malinzi ameiambia SALEHJEMBE kwamba ataendelea kulifuatilia suala hilo kwa karibu hadi siku atakapomkamata mtu mmoja atakayekuwa mfano kwa wengine wasiotaka kuachana na tabia hiyo.

“Rushwa ni jambo baya, linatukwamisha na kuvuruga kabisa juhudi zetu za kukuza mpira. Wako watu wanajihusisha na kila mara nimekuwa ninaonya.

“Inawezekana ninavyoonya wako wanadhani ni utani. Lakini siku nitamkamata awe mwamuzi, mchezaji au kiongozi, kwa kweli atajuta.


“Msisitizo wangu ni watu kuachana na kujihusisha na masuala ya rushwa ili tuendeleze mpira,” alisema Malinzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic