August 25, 2015


Na Saleh Ally, Kertepe
Ile mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Iraq iliyopangwa kupigwa kesho, haipo.


Mkuu wa Msafara, Msafiri Mgoyi amesema wameahirisha mechi hiyo kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.


“Mechi ya kesho haitakuwepo, imeahirishwa na Kocha Mkwasa ataendelea na proramu zake," alisema Mgoyi.

Mgoyi amesema mechi hiyo imeahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema baada ya kuahirishwa kwa mechi hiyo, wataendelea na programu nyingine kama kawaida.


“Kweli imeahirishwa ile mechi, sasa tutaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa vizuri,” alisema Mkwasa.

Stars inaendelea kujifua na leo asubuhi imefanya mazoezi makali kwa zaidi ya saa mbili na nusu.

Lengo la kambi ya hapa Uturuki ni kujifua kuhakikisha Nigeria 'wanakufa' katika mechi ya Septemba 5 jijini Dar es Salaam kuwania kucheza Afcon.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic