Simba imeendelea na
mchakato wake wa kusaka mshambuliaji ‘muuaji’ baada ya kumshusha nchini Makan
Dembele raia wa Mali.
Dembele tayari amepelekwa
Zanzibar kuungana na wachezaji wengine wa Simba walio huko ili apate nafasi ya
kumuonyesha Kocha Dylan Kerr kwamba yeye ni nani na ana uwezo upi.
Tayari mshambuliaji Pape
Abdoulaye N’daw raia wa Senegal naye yuko Zanzibar kufanya majaribio na Kerr ndiye mwenye
uamuzi wa mwisho kuweka tiki.
Dembele ,29, aliwahi pia
kukipiga katika klabu kongwe ya Algeria ya JS Kabylie.
Simba imeachana na
mshambuliaji Papa Niang raia wa Senegal pia baada ya kumpa siku mbili za
mazoezi pamoja na dakika 45 katika mechi ya kirafiki.
Imekuwa ikihaha kusaka
mshambuliaji mara tu baada ya kuachana na Amissi Tambwe ambaye ametua Yanga na
kuendelea kutesa.
0 COMMENTS:
Post a Comment