Baada ya kuzituliza Simba na Azam FC, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema sasa anaitaka Yanga.
Mwadui FC iliyopanda daraja msimu huu imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Azam FC na zote zimemalizika kwa sare.
Ilianza na Simba kwenye Uwanja wa Taifa na sare ikawa ya bila kufungana kabla ya sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC.
"Tumepata mechi hizo mbili ambazo tumepata sare mbili dhidi ya Simba na Azam. Si kwamba tunajisifia sare, lakini ninaangalia namna vijana wangu walivyocheza vizuri na tunapata nafasi ya kurekebisha makosa.
"Kweli tunawataka Yanga, tukifanikiwa nitafurahi kwa kuwa kitakuwa kipimo kingine bora kwetu kwa ajili ya maandalizi ya mwisho," alisema Julio aliyewahi kuwa kocha na mchezaji wa Simba kwa nyakati tofauti.
0 COMMENTS:
Post a Comment