August 28, 2015


Rais wa Simba, Evans Aveva, amevunja ukimya kuhusu majaaliwa ya fowadi Mkenya, Paul Raphael Kiongera ambaye yupo kwa mkopo KCB ya Kenya na kusema kuwa atarejea Msimbazi Desemba, mwaka huu.


Simba imekuwa ikihaha kusaka mfungaji, jambo ambalo limekuwa likizua maswali kwa nini hawamchukui Kiongera kama bado ni mchezaji wao?

Kiongera alisajiliwa na Simba msimu uliopita, lakini bahati mbaya hakudumu baada ya kuandamwa na majeraha mwanzoni kabisa mwa msimu alipoumia katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Coastal Union, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Simba ilimpeleka kwa mkopo KCB kabla ya kumrejesha hivi karibuni kwa ajili ya kuangalia ‘fitness’ yake lakini ilikuwa bado na akarejeshwa tena KCB.

“Bado ni mchezaji wetu, hatujamuacha na tutakuwa naye kuanzia Desemba,” alisema kwa ufupi Aveva.


Staa huyo aliwakosha mashabiki wa Simba katika mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ambapo alitupia kambani mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0, huku Ramadhan Singano ‘Messi’ akitupia jingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic