Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini (TRA) inatarajiwa
kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa klabu zilizopo jijini Dar es salaam,
siku ya ijumaa tarehe 14 Agosti katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la
Kisutu.
TRA itaendesha semina hiyo kwa klabu zilizopo ligi
kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa
vilabu hivyo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina
hiyo.
Kwa kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es
salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa vilabu vilivyopo mikoani kwa
lengo la viongozi wa vilabu kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji,
makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.
Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili
asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam,
vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili
waliopo jijini Dar es salaam mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment