KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS KILICHOPAMBANA NA KUREJEA LIGI KUU BARA. |
African Sports imeamka
baada ya kupata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara.
African Sports imeibuka
na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya ligi hiyo dhidi ya Ndanda FC.
Katika mechi hiyo kwenye
Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wageni walionekana kuwa imara zaidi kipindi
cha kwanza.
Hata hivyo, wenyeji
African Sports walijibu mapigo baada ya kuanza kipindi cha pili kwa kasi hadi
walivyopata bao.
Bao lao lilifungwa na
Hassan Matelema katika dakika ya 59 kupitia Hassan Matelema.
Baada ya bao hilo, Ndanda
walicharuka lakini mara kadhaa African Sports ambao walicheza kwa tahadhari
kubwa walikuwa wakijibu mapigo.
Kabla Sports ilicheza
mechi tatu na kupoteza zote, ikianza kufungwa bao 2-0 na Simba, ikasafiri hadi
Shinyanga na kufungwa tena kwa idadi hiyo na Mwadui.
Kabla ya mechi ya leo,
ilibaki Shinyanga safari hii kwenye Uwanja wa Kambarage, ikachabwa na Stand
United bao 2-o.
0 COMMENTS:
Post a Comment