Wakati wapenzi na mashabiki wa Yanga wakiendelea kusherehekea
ushindi waliopata juzi Jumamosi dhidi ya Simba, imefahamika kuwa chanzo cha
ushindi huo ni kiungo wao wa kimataifa kutoka Zimbabwe, Thabani Kamusoko.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa, Yanga iliitandika
Simba mabao 2-0 na kufanikiwa kuvunja mwiko wa kunyanyaswa na timu hiyo kwa
kipindi cha miaka miwili.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kuwa, busara za Kamusoko ndizo zilizosababisha wakaibuka na ushindi
katika mchezo huo.
Alisema Kamusoko alifanya kazi kubwa sana ya kuwatuliza wachezaji
wenzake wa Yanga, hususan Cannavaro mwenyewe na Kelvin Yondani ambao katika
dakika 15 za kwanza, walicheza kwa presha kubwa huku wakijichanganya kila
wakati.
“Baada ya Kamusoko kuona vile, alitutaka tutulie na tusiwe na
presha, tucheze kwa kujiamini kama siku zote na tukifanya hivyo lazima
tutashinda.
“Kusema kweli tulimsikiliza na tufakanya hivyo na mwisho wa siku
mambo yalikuwa mazuri kwetu na tukafanikiwa kuibuka na ushindi,” alisema
Cannavaro na kisha kuongeza kuwa anawashukuru viongozi wake wa Yanga kwa
usajili wa Kamusoko na Donald Ngoma, kwani kazi yao inaonekana uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment