Kipa wa zamani wa Reli ya Morogoro na Taifa
Stars, Hemed Mussa, amefariki dunia nchini Saudi Arabia.
Mussa aliyechezea Reli mwishoni mwa miaka ya
1980 na 1990, amefariki baada ya kutokea tukio la mahujaji takribani milioni
mbili kukanyagana kwenye Mji wa Mina karibu kabisa na Makka wakati wakiwa
kwenye hijja.
Marehemu Mussa alikuwa mmoja wa mahujaji
Watanzania waliokwenda kuhiji na awali ilielezwa wanne kati yao walifariki
kupitia taarifa ya Mufti, Abu Bakari Zubery ambaye yuko Makka.
Mmoja wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha
kwa jina la Said Mussa, alisema wamepata taarifa hizo kutoka kwa mwandishi wa
redio moja nchini ambaye yuko hijja pia.
“Kweli ametueleza ndugu yetu amefariki
dunia, hivyo tunaendelea kufuatilia zaidi kwa kuwa awali kulikuwa hakuna
uhakika huo. Hatukuwa na uhakika, lakini sasa tumethibitisha,” alisema.
Kocha
Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema: “Nilimjua vizuri sana
marehemu, alikuwa kipa mzuri sana. Alikuwa mwajiriwa wa reli lakini mwenye
kipaji uwanjani, ni masikitiko.”
Mahujaji wa Tanzania waliofariki na majina
yao kutajwa kwamba ni miongoni mwa 717 waliofariki dunia ni Mwanaisha Hassan
Juma, Mkungwe Suleiman, Hemed na Sefu Said Kitimla.
0 COMMENTS:
Post a Comment