Kiatu alichokitumia mshambuliaji wa
Simba, Paper Ndaw kiliwashangaza wengi kutokana na kuwa chakafu kwelikweli.
Kiatu hicho aina ya Adidas
kilionekana kimechoka vibaya na kuwashangaza wengi wakati akiingia Uwanjani
katika mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi.
Lakini katika mazoezi ya Simba kwenye
Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, Ndaw alionekana akiwa na ‘njumu’
mpya aina ya Puma.
Kiatu hicho aina ya Puma ni kipya
kabisa na Ndaw alikuwa akipiga tizi safi kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment