Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Dk John Magufuli, amewaahidi wanamichezo kuwa, endapo atapata nafasi ya kuwa
rais, atahakikisha anaweka mikakati ya kuzisaidia timu za hapa nchini zikiwemo
Yanga, Simba na Taifa Stars kuhakikisha zinakuwa mabingwa wa Afrika.
Magufuli alisema hayo juzi Jumatano alipokuwa
kwenye mkutano wa kampeni za kuomba kura za urais zilizofanyika katika Uwanja wa
Kawawa uliopo Kigoma Ujiji.
Mgombea huyo alionyesha mshangao kwa Tanzania
yenye watu zaidi ya milioni 50, kuzidiwa kisoka na nchi ndogo zenye wananchi
wachache.
“Haiwezekani wakazi wote hawa wa nchi yetu
tulivalie njuga suala la michezo kutoka katika kila kona ya nchi yetu halafu
baada ya muda fulani tushindwe kupata kikosi bora cha timu ya taifa.
“Suala la soka hapa nchini tunalikosea katika
msingi na viongozi wanachokitolea macho ni timu za juu, yaani tukisikia
michuano ya kimataifa kazi yetu ni kukimbilia timu zinazoweza kupata wachezaji
wa kuliwakilisha taifa wakati serikali yenyewe haijui mchezaji huyo hata
alivyolelewa mpaka kuteuliwa kuliwakilisha taifa,” alisema Magufuli na
kuongeza:
“Nawaahidi Watanzania katika utawala wangu
nitahakikisha nalisimamia suala la soka na michezo mingine kuanzia timu ndogo
kabisa za mchangani mpaka timu za ligi kuu.”
TUNACHEZA…
Wakazi wa Kasulu Mjini wakicheza ngoma iitwayo
Elijaki ambayo hutumika kuelimisha jamii kitaifa na kimataifa wakati
wakimsubiri mgombea wa urais kupitia CCM, John Magufuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment