Beki wa Tanzania Prisons, James Josephat
ameendeleza rekodi ya timu yake ya kutoa mchezaji wa kwanza kupata kadi
nyekundu katika Ligi Kuu Bara.
Beki huyo alipata kadi hiyo juzi baada ya
kumfanyia madhambi kiungo wa Yanga, Simon Msuva na kupewa kadi nyekundu akiwa
ndiyo wa kwanza msimu huu. Ilikuwa ni katika mchezo wao dhidi ya Yanga ambao
walifungwa mabao 3-0.
Msimu uliopita wa 2014/15, Prisons ndiyo walitoa
mchezaji wa kwanza kupata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Yanga ambao
walifungwa mabao 2-1.
Timu hizo zilikutana Septemba 28, 2014 katika
mchezo wa pili wa ligi hiyo ambapo beki wa Prisons, Jacob Mwaitalako alilimwa
kadi nyekundu akiwa mchezaji wa kwanza kupata kadi hiyo katika msimu huo.
Hivyo, Prisons imeweka rekodi kwa wachezaji wake
kwa msimu miwili kufungulia kwa kadi nyekundu, lakini pia michezo yote hiyo ni
dhidi ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment