Ushindi wa mabao 2-0 wa Yanga dhidi ya Simba juzi kwenye mechi ya
Ligi Kuu Bara, umewafanya wakoge mamilioni.
Yanga ilionja uhondo wa kuifunga Simba kwa mara ya kwanza tangu
Mei 18, 2013.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu
hiyo, wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo wamepewa kiasi cha shilingi
milioni 40 kama posho baada ya ushindi huo.
Chanzo hicho kilisema, wachezaji hao wamepewa kiasi hicho cha
fedha kutoka kwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji.
Kiliongeza kuwa, mgawo huo wa fedha hizo utawahusisha wachezaji
wote na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo.
“Kufuatia ushindi walioupata wachezaji wetu kwa kushirikiana na
benchi la ufundi, tumepanga kuwapa kiasi cha shilingi milioni 40 kama zawadi.
“Hiyo ni kama morali na pongezi kwa wachezaji wetu. Tuna kazi kubwa
katika kuhakikisha tunatetea ubingwa wa ligi kuu, ninaamini hilo linawezekana
kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wetu,” kilisema chanzo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment