Kuelekea
mchezo wa Yanga na Azam utakaopigwa
mapema Oktoba 17, mwaka huu, tayari timu hizo zimeanza mipango ya kujiandaa,
huku Azam FC ikisubiri wachezaji wake warejee kutoka timu za taifa na kwenda
kuweka kambi ya muda visiwani Zanzibar.
Msimu
uliopita awali, walitoa sare ya mabao 2-2, wafungaji wakiwa ni Amissi Tambwe na
Simon Msuva kwa Yanga huku Azam akifunga Didier Kavumbagu na John Bocco na mara
ya pili walipokutana, Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kikosi
cha Azam kimeanza mazoezi rasmi leo Jumanne katika uwanja wake wa Azam Complex,
ingawa asilimia kubwa ya wachezaji wapo katika timu zao za taifa.
Ofisa
habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema kuwa kikosi hicho kilianza mazoezi
jana Jumanne, licha ya wachezaji wengi kutokuwepo.
Kiongozi huyo alifunguka kuwa, wana mpango wa
kutafuta sehemu ya kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao, kama ni
hapa Dar au kwenda Zanzibar lakini itategemea na kocha atakavyoamua.
“Ni kweli mipango ya klabu na kocha wetu ni
kuhakikisha tunafanya vyema kwa kila mchezo na mchezo uliopo mbele yetu ni
dhidi ya Yanga na kama suala la kuweka kambi litakuwa ni pendekezo la kocha,
yeye ndiye ataamua kama ni hapa Dar au sehemu nyingine.
“Kwa sababu walioitwa timu za taifa wapo wa
nje pia kama Allan Wanga, ni vyema wakaungana pamoja na kuweza kuanza
maandalizi kwa pamoja ili kumrahisishia kazi kocha kutokana na kibarua
kilichopo mbele yetu, maana msimu huu hakuna timu ya kuidharau, zote
zimejipanga,” alisema Idd.
0 COMMENTS:
Post a Comment