October 17, 2015


Malimi Busungu, amesema ana uhakika atasababisha mchezaji wa Azam FC kulambwa kadi nyekundu katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo.


Yanga na Azam zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika uwanja huo jijini Dar es Salaam, lakini Busungu amesema kwa historia amekuwa akisababisha kadi nyekundu kila anapocheza dhidi ya Azam.

Busungu akiwa Mgambo JKT kabla ya kujiunga na Yanga, msimu wa 20013/14 alisababisha kadi nyekundu kwa Erasto Nyoni aliyemchezea vibaya, pia msimu uliopita Aggrey Morris alipatwa na tukio kama hilo.

Mshambuliaji huyo amesema: “Nina historia kila nikikutana na Azam katika ligi, mchezaji wao anapata kadi nyekundu kwa kunichezea vibaya, natabiri Jumamosi (leo) itatokea hali hiyo.”

Busungu alisema anajua namna mabeki wa Azam wanavyocheza kwa kutumia nguvu kupita kiasi lakini atahakikisha anafanya vizuri mbele yao endapo atapata nafasi ya kucheza.


Wakati huohuo, Busungu alisema; “Nafurahi kucheza pamoja na Ngoma kwani hata yeye ameniambia anapenda kucheza kikosi kimoja na mimi kwa kuwa anavutiwa na uchezaji wangu wa kupambana.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic