October 17, 2015

MINGANGE AKIBADILISHANA MAWAZO NA MSHAMBULIAJI WAKE MPYA, HARUNA MOSHI 'BOBAN'.

Kaimu Kocha Mkuu wa Mbeya Citym Meja Mstaafu Abdul Mingange amefanya kitu kimoja cha kuwashtua wapinzani wake Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.


Mingange ambaye anaiongoza Mbeya City kwa mara ya kwanza akikaimu nafasi ya kocha mkuu baada ya kuondoka kwa Juma Mwambusi, alisema amebadili mfumo wa ulinzi ili Simba isipate bao kirahisi.

Alisema: “Nitachezesha mabeki wa kati watatu badala ya wawili kama ilivyozoeleka, unajua nataka tusifungwe kabisa na Simba na hata tukiruhusu mabao basi yasiwe mengi ila lengo ni ushindi.”

Ili kutekeleza mpango huo, Mingange amepanga kuwatumia mabeki Yohana Morris ambaye ni mdogo wa nyota wa zamani wa Prisons, Osward Morris na Herry Morris na Haruna Shamte ambao watakuwa pamoja na kiungo mkongwe Steven Mazanda.


“Mazanda ni kiungo lakini nitamtumia kama beki wa kati anayechezesha timu huku akilinda sana, pale mbele watasimama Themi Felix na Boban (Haruna Moshi) hapo kazi imeisha,” alisema Mingange aliyewahi kuzinoa Ndanda FC na Villa Squad.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic