October 17, 2015


Mshambuliaji Hamis Kiiza leo anaweza akaitumikia timu yake kwenye Uwanja wa Sokoine wakati ikiivaa Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara.


Ingawa kumekuwa na taarifa kwamba Kiiza ni majeruhi, taarifa za ndani kutoka Simba zimeeleza Kiiza tayari amerejea ingawa wamekuwa hawataki kuweka mambo hadharani.

Imeelezwa Kiiza atakuwa kati ya wachezaji 11 watakaoanza leo katika kikosi cha Simba.

“Kama itashindikana, basi ataanzia benchi lakini ana uhakika wa kuingia,” kilieleza chanzo.

“Juhudi kubwa za kimatibabu zimefanyika na sasa Kiiza yuko katika hali nzuri.”


Kiiza raia wa Uganda ndiye mfungaji mwenye mabao mengi zaidi Simba baada ya kuwa amepachika matano na ndiye anaongoza pia katika waliofunga mengi katika Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic