October 8, 2015


Mgombea ubunge wa CCM kwa jimbo la Moshi Mjini ni Davis Mosha, si unamkumbuka?


Mosha aliwahi kuwa mmoja wa viongozi wa Moro United, baadaye akashinda uchaguzi na kutwaa kiti cha Makamu Mwenyekiti wa Yanga, kabla ya kujiuzulu.


Jana alilazimika kupanda jukwaani kucheza nyimbo zote za kundi la Tip Top Connection likiongozwa na Rais wa Manzese, Madee na Tunda Man.
Baada ya hapo, akakamua tena nyimbo za Yamoto Band, hehe chezea kampeni wewe.


Kama haitoshi, Mosha akataka kuonyesha yuko fiti baada ya kupiga zile push up za “Magufulika”, hata hivyo alikuwa hoiii.

Mosha ni kati ya wanaopewa nafasi ya kushinda katika jimbo hilo la Moshi mjini ambalo aliyekuwa mbungwe wake, Philemon Ndesamburo kutoka Chadema aliamua kutogombea.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic