Taifa Stars imeanza vizuri kampeni ya kuwania
kucheza Kombe la Dunia baada ya kuitwanga Malawi kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, Stars ilipata mabao yake yote mawili katika kipindi
cha kwanza.
Bao la kwanza, lilitipiwa kimiani mapema tu na
Mbwana Samatta ambaye alikuwa mwepesi kuiwahi pasi maridadi ya Thomas Ulimwengu
na kufunga kwa ustadi mkubwa.
Ulimwengu, safari hii akipata ‘zawadi’
kutokana na kumfuatilia kipa wa Malawi aliyeutema mpira wa krosi wa Haji
Mwinyi.
Hata hivyo, Malawi walionekana matata zaidi
katika kipindi cha kwanza mwanzo wakitawala dakika zote 15 za mwanzo.
Stars ikageuka na kutawala dakika zote za katikati kabla ya wageni kurejea na kutawala kipindi cha pili mwishoni.
Kipindi Kocha Charles Boniface Mkwasa akiwa
anaingoza Stars kwa mara ya kwanza akiwa Kocha Mkuu mwenye mkataba, aliwatoa
Mrisho Ngassa akamuingiza Salum Telela na Simon Msuva akaingia badala ya Thomas
Ulimwengu.
Mchezaji mwingine aliyeingia ni Ibrahim Ajibu
na kufufua nguvu ya ushambuliaji ya Stars.
Hata hivyo, katika kipindi cha pili Stars
walitoa nafasi nyingi zaidi kwa Malawi kushambulia zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment