October 21, 2015


Pamoja na kuwa na wachezaji wengi  bora katika kikosi cha PSG, Angelo Di Maria anaonekana kuwa tishio kwa Real Madrid.

Madrid inakutana na PSG katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayotarajiwa kuwa kali sana.


Mechi hiyo inayopigwa leo jijini Paris inaonekana kuwa gumzo na Di Maria ambaye amewahi kuitumikia Madrid, ndiye anaelezwa atakuwa tatizo.

Di Maria raia wa Argentina anaonekana kuwa atatumika kama sehemu ya kusukuma mashambulizi kutokea pembeni.

KAsi yake, uwezo wa kupiga chenga na krosi zenye ‘macho’ ndiyo zinaonekana zitakuwa tatizo kwa Real Madrid.


Hata hivyo Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez amesema wako tayari kwa kulinda na wanachotaka ni kufunga mabao na kushinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic