October 25, 2015


Divock Origi ni Mkenya, lakini ana uraia wa Ubelgiji. Sasa anakipiga Liverpool. Victor Wanyama pia ni Mkenya na anakipiga Liverpool.

Utaona picha inaonyesha wawili hao wakikabana katika mechi ya Ligi Kuu England iliyoisha kwa sare ya 1-1.

Nataka Mtanzania ujiulize, vipi Watanzania wanashindwa kufika hapa?
Kweli ni sahihi, tatizo ni viongozi, wachezaji wenyewe au mazoea?

Nani anatakiwa kurekebisha hili? Lazima tuone aibu na kuondoka hapa.


Wakenya ambao karibu kila kitu tunafanana, wanatuzidi katika riadha, soka, rugby na wanaingiza fedha nyingi sana. Sasa wachezaji wao wanazidi kusambaa duniani kote. Sisi tupo hapa, hakuna maendeleo zaidi ya majungu na kusutana tu. Mwisho wetu utakuwa wapi? Tujiulize mara nyingi sana.

Kama ni mchezaji, kocha au kiongozi unayependa maendeleo, picha hii itakusuta na utabadilika na hatua tutapiga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic