Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma
salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha
aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana
mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa,
marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini,
kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu
Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika
nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu
Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa
niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole
wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment