October 26, 2015


Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuitandika Yanga.

Mwadui FC ya mkoani Shinyanga inaikaribisha Yanga mjini humo keshokutwa Jumatano katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Julio amesema Mwadui FC itakuwa ya kwanza kuifunga Yanga ambayo imecheza mechi mfululizo bila ya kufungwa.

“Timu yetu ilianza kwa kuonekana haifai, ilizdhauliwa na wengi walisema ni timu ya wageni.

“Lakini sisi ni watu tunaojua cha kufanya na utaona Yanga watakachokutana nacho,” alisema Julio.
“Tunajiamini, hata kama tunaheshimu uwezo wa Yanga lakini tuna kikosi bora kabisa,” alisema Julio.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic