October 26, 2015



 Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameibuka mshindi katika nafasi ya udiwani kwenye eneo la Mbagala Kuu.


Taarifa za kutoka katika kituo cha uchaguzi zimeeleza kwamba Manji ameshinda mara mbili ya mpinzani wake.

“Ni kweli ameshinda, lakini kila kitu tayari tumebandika pale,” alisema mmoja wa wasimamizi.

Hata hivyo ilitarajiwa kwa Manji kuibuka na ushindi ingawa kuna taarifa zinaeleza wapiga kura nusu hawakujitokeza kutokana na kuona ni lazima Manji atashinda na hakuwa na mpinzani.

Mgombea maarufu kutoko wote wa udiwani alikuwa ni Manji ambaye alionekana angeweza kugombea ubunge badala ya udiwani kutokana na umaarufu wake kuwa mkubwa zaidi kuliko wagombea wote wa udiwani nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic