October 18, 2015


Kamati ya Taifa Stars chini ya Mwenyekiti, Faroukh Baghoza imekutana usiku huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Kamati hiyo imekutana ikiwa ni kwa ajili ya kupanga mikakati pamoja na kuunda kamati ndogondogo.
MWENYEKITI WA KAMATI, FAROUKH BAGHOZA (KULIA) AKIWA NA MICHAEL WAMBURA NA JUMA PINTO.
Kamati hiyo pia ilitoa nafasi kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa maoni yao kwa lengo la kuhamasisha na kuisaidia Taifa Stars kuitoa Algeria katika mchakato wa kuwania kucheza Kombe la Dunia, Novemba.

Stars inawania kucheza Kombela Dunia nchini Urusi mwaka 2018 na sasa itakutana na Algeria ikiwa ni baada ya kuitoa Malawi.

KATIBU TEDDY MAPUNDA NA FAROUKH.

Katika mkutano huo chini ya Baghoza na katibu, Teddy Mapunda, kamati hiyo iliwapa wadau wakiwemo waandishi wa habari kutoa maoni yao katika masuala kadhaa yakiwemo ya uhamasishaji kwa Watanzania.

Mengi yalizungumziwa na baada ya hapo, mapendekezo hayo yatapelekwa kwenye kamati ndogondogo ambazo zitagawanya majumu ili kuharakisha utendaji.
MUSLEY AL RUWEY AKIWA NA HASSAN

Lengo kuu la kamati hiyo ni kusaidia kufanikisha ushindi kwa kuviong’oa vigogo, Algeria ambao ndiyo timu bora Afrika kwa kipindi hiki.

SALEH ALLY 'JEMBE' NA EDO KUMWEMBE.



KATABALO...

IMANI MADEGA, MAULID KITENGE NA SALIM TRYAGAIN

MSAFIRI MGOYI, BARAKA KIZUGUTO NA ISSAC CHANJI

MOHAMMED NASSOR 'KIGOMA', PINTO NA WAMNBURA

MULAMU NG'AMBI NA HASSAN





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic