Mechi za raundi ya 11 za Ligi Kuu Bara zilizokuwa
zichezwe Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika Desemba 12 na 13 kupisha
maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni
kati ya Mgambo Shooting na Yanga (Tanga), Kagera Sugar na Ndanda (Tabora),
Stand United na Mwadui (Shinyanga), Mbeya City na Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam na
Simba (Dar es Salaam) na Majimaji na Toto Africans (Songea). Mechi za Desemba
13 ni kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons (Dar es Salaam), na Coastal Union na
African Sports (Tanga).
Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa
Oktoba 4 mwaka huu kupisha mechi ya Taifa Stars na Malawi sasa zitafanyika
Desemba 16 mwaka huu. Mechi hizo ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam),
na African Sports na Yanga (Tanga), mchezo kati ya Ndanda na Simba (Mtwara
utapangiwa tarehe ya kuchezwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment