N'DAW |
Wakati wadau wa soka nchini wakiponda uwezo wa
straika Papa N’daw katika kikosi cha Simba, kocha wa timu hiyo, Dylan Kerr
amesema aliyekuwa nje hawezi kuona umuhimu wa mchezaji huyo lakini ni mtu
muhimu kikosini.
Kerr alienda mbali kwa kusema; “Straika si
lazima afunge, huyu mnamponda lakini mimi ndiye ninayejua umuhimu wa mchezaji
huyu kikosini.”
N’daw mshambuliaji mrefu kuliko wote katika
Ligi Kuu Bara amesajiliwa kwa mkopo Simba akitokea Dinamo Bucuresti ya Romania,
bado hajaonyesha makali yake kiasi watu kutilia shaka uwezo wake.
Akizungumzia na Championi Jumamosi, Kerr raia
wa Uingereza, alisema licha ya kutofunga hadi sasa, straika huyo ni msaada
mkubwa kikosini kwa kuisaidia timu kupata ushindi na pia kuelewana uwanjani.
“N’daw kwanza ni mchezaji mgeni anahitaji muda,
yeye ni msaada mkubwa katika timu, mara nyingi ni mtu wa kusafisha makosa ya
timu, anaweza kukaa na mpira na kuwatengenezea wengine nafasi wakafunga,”
alisema Kerr.
0 COMMENTS:
Post a Comment