October 7, 2015


Pamoja na juhudi kubwa ya kusajili wachezaji, Liverpool ndiyo timu kubwa inayosuasua zaidi hadi sasa katika msimu huu wa Ligi Kuu England.


Licha ya mabingwa watetezi Chelsea kuwa katika hali mbaya zaidi, lakini Liverpool imelazimika kumfukuza Kocha Brendan Rodgers baada ya kuona hakieleweki.
Imecheza mechi nane na kukusanya pointi 12 na iko katika nafasi ya 10.
Mjadala uliopo kwamba ni kweli wachezaji wa bei lahisi waliiangusha Liverpool ambayo ilisajili wachezaji 7 na kuwa moja ya timu zilizosajili sana!
Lakini ikashindwa kufanya vema kwa kuwa wachezaji wake wengi walianza pauni milioni 15 hadi 25.

Lakini haikuwa lahisi kupata wachezaji wengi kuanzia pauni milioni 25 kwenda juu, jambo ambalo baadhi ya wachambuzi wanaona wachezaji hao wa ‘kuchangisha’ ilikuwa ni moja ya sababu ya Liverpool kutokuwa na mwendo mzuri.


Sasa ni zamu ya Kocha Jurgen Klopp aliyewakuwa kocha wa Borussia Dortmund kuonyesha kama ni kweli au la ingawa kocha huyo anasifika kwa kuwajenga wachezaji wenye majina madogo hadi kuwa nyota na wenye msaada mkubwa kwa kikosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic