Sraika wa Yanga, Amissi Tambwe,
ameyakomba mamilioni ya Simba baada ya uongozi wa timu hiyo kukamilisha malipo
yake ya zaidi ya shilingi milioni 14 aliyokuwa akidai baada ya kukatisha
mkataba wake msimu uliopita.
Tambwe aliachwa Simba katika msimu uliopita
kwenye dirisha dogo kufuatia kudaiwa kuwa, aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrick
Phiri alimkataa katika kikosi chake kwa madai ya kushindwa kuendana na mfumo
wake. Hata hivyo, Phiri alikanusha, akidai viongozi wenyewe ndiyo waliomkataa.
Mchezaji huyo ambaye amefunga mabao
manne kwenye ligi hadi sasa, alikuwa akiidai Simba dola elfu 7,000 ambazo ni
zaidi ya shilingi milioni 14 kufuatia kukatishwa kwa mkataba wake wa miezi sita
ambapo alikuwa akilipwa mshahara wa milioni moja na nusu kwa mwezi.
Tambwe amesema kuwa, tayari ameshamalizana na Simba kwa kumlipa fedha zake zote
kupitia mapato ya mlangoni, japokuwa ilikuwa tabu sana kupata malipo hayo.
“Ni kweli tayari nimeshamalizana na
Simba kwa kunilipa fedha zangu zote nilizokuwa nikiwadai kutokana na
kunikatishia mkataba wangu, japokuwa ilikuwa mbinde kunipa.
“Kwa sasa siidai klabu hiyo na
ninachoangalia ni jinsi gani naweza kuisaidia timu yangu ya Yanga iweze
kufanikiwa kufanya vyema na hatimaye kutetea ubingwa wetu,” alisema Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment